Advertise Here

Saturday, September 14, 2013

Aliyekuwa Kahaba kisha kuokoka na kuwa Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, aeleza sababu za kuwa Kahaba.

Caroline Sam a.k.a Maheeda
Caroline Sam a.k.a Maheeda, Raia wa Nigeria aliyeacha ukahaba na kuamua kuokoka kisha kuwa Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, aelezea sababu za watu kuwa makahaba baada ya yeye kufanya ukahaba kwa muda mrefu, hata baada ya yeye kufunga ndoa.

Mtoto wa Maheeda
Maheeda anasema "... Hata baada ya kufunga ndoa, mimi bado nilikuwa natoka nje ya ndoa. Lakini nilihisi ni lazima kuwa hivyo. Ninachotaka watu wajue ni kuwa kuna roho nyuma ya ukahaba, kama siyo, kwa nini mimi baada ya kufunga ndoa, na nilikuwa na kila kitu yaani naishi Lekki, nilikuwa naendesha gari kubwa sana, mume wangu alikuwa akinipa chochote nilichokuwa nataka, lakini bado nilikuwa nafanya ukahaba. Kuna roho nyuma yake. Mimi niliendelea na ukahaba hata baada ya kufunga ndoa. Jambo moja tu lililonibadilisha mimi ni kuokoka na kufunguliwa".