Advertise Here

Friday, March 15, 2013

Bony Mwaitege: Nafurahi kuwa na Matunda yangu.

Bony Mwaitege
Na; Dennis Nyali

Mwimbaji wa nyimbo za injili Bony Mwaitege amesema kuwa hana ugomvi na waimbaji chipukizi wanaotamani kuwa kama yeye katika huduma ya uimbaji. Bony ameyasema hayo katika kipindi cha Overcomers Show kinachoendeshwa na Mtangazaji Denis Nyali katika kipengele cha Tripple stage kupitia kituo cha Radio cha Overcomers Fm.

Bony amesema "Mimi nashukuru kama kuna watu wananikubali na kufanya kama mimi na hatakama watafanya vizuri zaidi yangu, kwangu itakuwa ni furaha kwani yatakuwa ni matunda yangu."

"Unajua mtangazaji mziki hauna mwenye nao kwa sababu magitaa yanayotumika ni yaleyale na vinanda ni vilevile kwa hiyo kuigana kwa beat au wimbo ni kitu ambacho hakiwezi kukwepeka mbona watu wanaiga sauti za watu mbalimbali kama vile Kikwete, Nyerere na viongozi wengine kwahiyo mimi watu kuniiga namshukuru Mungu kwa hilo pia". Aliongeza Bony. 

Hata hivyo Bony amesema watu wengi wanasema yupo kimya lakini anajipanga kuja kivingine na anatarajia mwezi wa tano au wa sita kuachia albam yake ya tatu huku albam yake ya mama ni mama na utanitambuaje zikiendelea bado kufanya vizuri.