Advertise Here

Friday, March 15, 2013

Holly Gospel Search kuanza kutikisa Iringa.

Na; Dennis Nyali

Mchakato wa kutafuta vipaji katika mkoa wa Iringa maarufu kama Holly Gospel Search, umeanza rasmi huku washiriki wakiwa na hamu kubwa ya kuwania zawadi mbalimbali kama vile kurekodi Albamu pamoja na zawadi nyinginezo.

Katika kuhakikisha vijana wanasaidiwa kutoka katika hali duni za kimaisha, Mkurugenzi wa Band ya Muziki wa Injili ya Jesus My Life Bi. Kazinyolo, ameandaa shindano hilo maalumu kwa ajili ya kutafuta waimbaji chipukizi wa Muziki wa Injili wenye vipaji.

Shindano hilo lilianza rasmi Machi 9, 2013 kwa usaili na kuanza rasmi kwa Mchujo Jumamosi hii yaani Machi 16, 2013 ambapo zaidi ya vijana 30 wanatarajiwa kuwania nafasi mbali mbali siku hiyo.  

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii Mkurugenzi huyo amesema kuwa lengo la kuandaa shindano hilo sio kuibua vipaji pekee bali ni kuwafanya vijana waweze kuhubiri Injili zaidi kupitia uimbaji kwani kuna shuhuda mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kuhusu watu kuokolewa kwa njia  ya uimbaji. 

Kwa upande wa washiriki wamemshukuru sana Mkurugenzi huyo kwa kutambua kuwa kuna watu wamesahaulika na kujiingiza katika matendo maovu  ambayo yangesababisha kuongezeka kwa Matendo maovu katika jamii na kupelekea maambukizi ya vvu.

Hizi ni Baadhi ya Picha za washiriki waliofika Siku ya Kwanza ya Usaili
 
 
 
Mashindano hayo yanatarajia kuendelea Jumamosi hii Machi 16, 2013.