Advertise Here

Saturday, March 2, 2013

Mambo ya kuangalia katika Msichana afaaye kuwa Mke.


VIJANA wengi wamekuwa wakikimbilia Ndoa pasipo kujua ni vitu gani vya Msingi wanatakiwa kuzingatia kabla ya kufika hatua ya Kufunga ndoa. Sasa leo tutazame Mambo ya Msingi ya Kuangalia katika Msichana afaaye kuwa Mke.

Kijana Mvulana na achague msichana ambaye atasimama imara kando yake na ambaye ataweza kuchukua sehemu yake ya mzigo wa maisha. Mke ambaye mvuto wake utamfanye mumewe kuwa na Heshima na kumwezesha kuwa na mwenendo mwema, na ambaye kwa ajili ya upendo wake, atamfanya kuwa na raha maishani mwake.

“Mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”. Moyo wa mumewe humwamini……………! Humtendea mema wala si mabaya, siku zote za Maisha yake. Hufumbua Kimya chake kwa Hekima, na Sheria ya wema I katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uvivu.

Wanawe huondoka na kumwita heri, mumewe naye humsifu, na kusema binti za watu wengi wamefanya mema, lakini wewe umewapita wote. “Yeye apataye mke wa namna hiyo, apata kitu chema; naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Hebu vijana na wajishauri kwa uangalifu mkubwa kuhusu mambo haya yafuatayo, na bila shaka kama yakizingatiwa kwa makini yatakuwa Msaada mkubwa kwa mvulana mwenye nia ya kuoa; Je! Yule unayekusudia kumuoa atafanya Nyumba yenu iwe na furaha? 

Yeye ni Mwangalifu awezaye kutunza Mali zenu? Au ni mtu ambae hutawanya Mali kipumbavu huku akionyesha Upendo wa Juu Juu tu? Mwenendo wake alionao ukoje kwa wakati huu? Anacho kitu chochote akitumainicho kwa wakati huu?

Nafahamu kwamba Mvulana ambaye ametumbukia katika Kisima cha Mapenzi, atayadharau Maswali haya kana kwamba hayana mana wala manufaa yoyote lakini hayana budi kufikiriwa kwa uangalifu Mkubwa iwezekanavyo.

Wakati wa kuchagua Mke, tafakari na uelewe tabia na Mwenendo wa Mwanamke unayetaka kumuoa, ili uone kama atakuwa Mstahimilivu na Mwenye bidii. Uone kama atachoka kuwatunza wazazi wako walio wazee wakati ule watakapokuwa wanahitaji Msaada wako.

Uone kama atakutenganisha nao na kukushawishi umpende yeye peke yake na kutumikia Starehe zake tu, na kukufanya uwasahau Baba na Mama yako ambao badala ya kupata binti, watakuwa wamepoteza Mwana. 

Kesho tutakuletea Mambo ya Kuangalia Katika Mvulana afaaye kuwa Mme.

 - Ellen G. White -