Advertise Here

Monday, March 4, 2013

Mambo ya Kuangalia katika Mvulana afaaye kuwa Mme.

 
JANA tulielezea Mambo ya kuangalia katika  Msichana afaaye kuwa Mke. Sasa leo tutazame Mambo ya kuangalia katika  Mvulana afaaye kuwa Mme.

Kabla Msicha yeyote hajatoa mkono wake kwa Mvulana, kwanza na ajiulize kama Yule mvulana wanayekaribia kuoana anafaa ama vipi. Mwenendo wake na tabia yake ya Siku zilizopita ilikuwa ya namna gani? Maisha yake ni Masafi? Upendo anioneshao unatoka Moyoni na Unaonesha heshima na tabia njema? Ama ni Upendo wa hivi hivi tu?

Anao mwenendo ambao utanifanya kuwa na Furaha? Mimi kama Mke nitaweza kuwa na Furaha niwapo kwake? Ataniruhusu kudumisha tabia yangu nzuri na kunipa Uhuru, ama itanilazimu kutupilia mbali yote na kuangukia katika Mamlaka yake?

Nikiwa nae kama Mme wangu, nitaweza kumuheshimu Mwokozi wangu kama Mkuu katika yote? Mwili na Roho, Matendo na Mawazo vitaweza kuhifadhiwa katika hali timilifu na takatifu? Maswali haya kama yakizingatiwa kwa Busara yatakuwa ya Manufaa sana katika Maisha yajayo ya Msichana anayetarajia kuolewa.

Kila Msichana anayetumainia kuwa na familia yenye furaha na Amani ambayo haitajua Udhaifu wala Huzuni katika siku za mbele na ajiulize Maswali haya kabla ya kutoa ukubali wake wa Upendo. 

Je! Mpenzi wangu ana Mama? Tabia ya Mama yake ikoje? Anatambua wajibu wake kwa Mama yake? Anajali Upendo na Furaha ya Mama yake? Ikiwa hajali wala Kumuheshimu Mama yake, Je! Kweli ataweza kuonyesha Heshima na Upendo, Wema na Usikivu kwa Mkewe?

Shani ya harusi itakapokwisha, atakuwa na Huruma kwa Makosa yangu ama atakuwa akinikosoa mara kwa mara akiwa Mgomvi na Mkali? Katika kuyajibu Maswali haya, shauku nyingi yaweza kupishia Mbali Makosa na Kasoro za Mchumba wako lakini Upendo wa kweli hautaficha Neno.

Mkubali afaaye kwa Tabia
 Katika kuchagua Mwenzi wa Maisha, Msichana na achague Mvulana aliye na Tabia na Mwenendo safi wa kibinadamu, aliye na bidii, Mwangalifu, Mwenye heshima, na aliye Mwaminifu na mnyoofu. Yule ampendaye na kumuogopa Mungu.

- Ellen G. White -