Advertise Here

Wednesday, October 31, 2012

Boko Haram waua waumini 7 wa Kanisa Katoliki Nchini Nigeria.

http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2012/10/Nigeria5.jpg
Mji wa Kaduna Nchini Nigeria
 TAKRIBAN watu saba wameuawa nchini Nigeria na wengine wengi wakijeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga katika kanisa la kikatoliki Kaskazini mwa Nigeria.

Maafisa wanasema kuwa gari lililokuwa limebeba mabomu liliingia katika kanisa hilo na kulipua mabomu huku athari zake zikitoboa shimo katika paa la kanisa hilo.

Shambulio hilo lilitokea mjini Kaduna, eneo ambalo limekuwa likilengwa sana na wapiganaji wa Boko Haram kwa mashambulizi katika siku za hivi karibuni.

Rais Goodluck Jonathan ameahidi kongeza juhudi za kupambana na ugaidi na vurugu nchini humo. Aidha Rais Goodluck alitaja shambulizi hilo kama kitu kisicho kubalika na ambacho kinatishia usalama na uthabiti wa nchi hiyo.

Mwandishi wa BBC mjini huko aliarifu kuwa shambulio hilo lilitokana na bomu lilotegwa kwenye gari lililopuliwa na mtu aliyejitoa mhanga na kugonga gari hilo kwenye ukuta wa kanisa.

Anasema uharibifu mkubwa ulitokea ndani ya jengo na kwamba mapaa ya maduka na nyumba za karibu yaling’oka.

Afisa mmoja wa kanisa hilo alisema watu kama wanne waliuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Kumetokea mashambulio kadha ya kidini katika jimbo hilo, mengi yamefanywa na kundi la wapiganaji wa kiislamu, Boko Haram.