Advertise Here

Monday, October 15, 2012

Revival Flames Campus Night ya Tafes Saut ni Ijumaa Hii Viwanja vya Shule ya Msingi Nyamalango.

TAFES tawi la Chuo Kikuu cha Mt. Agustino - Mwanza Campus wakishirikia na Radio ya Kikristo ya Alive Fm(91.9Mhz) na Kanisa la High Way of Holiness Cathedral chini ya Mpakwa Mafuta wa Bwana Bishop Eugene Murisa, wanakuletea Usiku wa Kusifu na Kuabudu uliopewa Jina la Revival Flames Campus Night.

Tamasha hili litafanyika Ijumaa ya Wiki hii kuanzia mida ya Saa 2:30 usiku katika Viwanja vya shule ya Msingi Nyamalango, pembezoni mwa Chuo Kikuu cha Mt. Augustino.

Akiongea nami Katibu Mkuu Tafes tawi la SAUT Bw. Remmy Paschal amesema kuwa Maandalizi yote ya Tamasha hilo yamekwisha kamilika na inasubiriwa siku hiyo tu ifike ili watu wasifu na kuabudu.

Mnenaji katika Tamasha hilo atakuwa ni Askofu Eugene Murisa kutoka Kanisa la High Way of Holiness Cathedral lililopo maeneo ya Ilemela Kanisani, Njia kuu ya kuelekea Airport.

Kwaya na Band mbalimbali zitahudumu wakiwemo TAFES Praise & Worship Team, Kingdom Worship, TAFES Choir, HHC Praise & Worship Team, Revival Mission Band(Wana wa Uzao wa Daudi) na  Wengine wengi.

Watu wote mnakaribishwa bila kujali dhehebu wala dini!
Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Katibu Mkuu wa Tafes Bw. Remmy Paschal Kwa Namba;
0757 194776 au 0712 355455