Advertise Here

Wednesday, October 24, 2012

Dotnata Posh sasa Kufungua Kanisa.

Dotnata Posh
MWIGIZAJI na aliyewahi kuwa Mwanamuziki Dotnata Posh, amesema kwa sasa ameaokoka kabisa na kuamua kufungua kanisa kubwa lengo likiwa kuwashawishi wasanii wenzake kuachana na  maasi na hatimaye kumrudia Mungu.

Dotnata ambaye alianza kwa kufafanua jina lake, alisema watu wengi wamezoea kumwamwita jina hilo bila kujua msingi wake, kwamba yeye jina lake ni Doto na ameunganisha na jina lake la ubatizo Illuminate ambapo akachukuwa jina la kwanza la Dot na kuunganisha jina la mwisho na  nate na kupata Dotnata.
T.B Joshua

Safari yake ya Nigeria
Dotnata anasema aliamua kwenda Nigeria  kwa Mtume T.B Joshua ambaye ni maarufu sana Afrika na Dunia nzima, ili kwenda kuchukua baraka kwaajili ya kuanzisha Kanisa hilo.

Alisema baada ya kurudi kutoka Nigeria na kupata baraka hizo za kufungua kanisa, hivi sasa anasomea masomo ya Biblia ili baadae aje kuwa  Mchungaji. Kwasasa yeye ni Mama wa Kanisa. Aidha aliongeza kwa kusema kuwa, kwa sasa kanisa lake litakuwa na wahubiri kutoka Nchi mbalimbali na baada ya hapo ataanza kutoa elimu kwa wasanii waweze kuokoka ili kumrudia Mungu.

Dotnata pia amesema kwa sasa hawezi kumlaumu msanii ambaye anafanya mambo ya ajabu ajabu kwakuwa anaamini ni ujana unamsumbua na ukifika muda atabadilika. Alizidi kusisitiza kuwa katika Kanisa lake anategemea pia kuwachukua wasanii Ray C na
Asha Madinda, ambao nao wameokoka.

Mwisho alimalizia kwa kusema Kanisa hilo kwa hivi sasa lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili, ingwa pia limeruhusiwa kuendelea na kazi zake za ibada.


- Bongo Unit -