Advertise Here

Sunday, October 14, 2012

Yaliyojili kwenye Changers Conference na Pastor Zakayo Nzogere wa MICC.

Pastor Zakayo Nzogere (Mnenaji)
 JANA katika hotel ya Victoria Annox iliyopo maeneo ya Furahisha jijini Mwanza, ilifanyika Semina ya Changers Conference chini Mtumishi wa Mungu Pastor Zakayo Nzogere ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Mwanza International Community Church(MICC).
Kufurahi pia kulikuwepo
Semina hii iliandaliwa na Vijana wa Kanisa la MICC ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kuandaa Semina kama hizi kwa vijana ili kuwajenga Kiroho na kimwili pia.
Vijana wakifuatilia Semina kwa Makini
Mada katika Semina hiyo zilikuwa ni mbili ambazo ni; Mahusiano(Urafiki, Uchumba hadi Ndoa) na Fursa za kimasomo nje ya Nchi.
Semina ikiendelea
 Leo Semina hii itakuwa katika Ukumbi wa Gandhi Hall uliopo karibu na Jengo la CCM Mwanza.
Kamati ya Maandalizi ya Semina



NYOTE MNAKARIBISHWA!!!
(Picha; Baraka Samson)