Advertise Here

Friday, October 12, 2012

Mbagala kwachafuka, mpaka sasa makanisa mawili yameshaharibiwa.

Polisi wakiwa eneo la tukio mbagala
BAADA ya kijana mmoja kukojolea Quran maeneo ya Mbagala Kizuiani-Dar es salaam, waislam katika jiji la Dar es salaam maeneo ya Mbagala wameandamana na kuharibu makanisa yaliyopo maeneo hayo.
Taarifa zinasema kuwa mpaka sasa Makanisa mawili yamevamiwa na Waislam na Kuharibiwa pia wameingia ndani ya Makanisa hayo na kuvunja vyombo vya muziki vya makanisa hayo. Makanisa hayo ni TAG pamoja na Kanisa la Kilutheri yote ya Mbagala.
Magari mawili yamevunjwa vioo na pia Maduka mengi yamefungwa huko Mbagala kuepusha madhara zaidi kutokana na vurugu hizo.
Tutawajuza mengi zaidi kadri tunavyozidi kupokea taarifa toka eneo la tukio.
 Picha; Masanja Mkandamizaji