Advertise Here

Sunday, October 14, 2012

Kutoka Maktaba: Mwl. Nyerere akipokea Sakramenti ya Meza ya Bwana toka kwa Papa John Paul II.

LEO ni siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Mwl. Julius Kambarage Nyerere, ambaye ni Rais na Waziri Mkuu wa Kwanza Nchini Tanzania. Miaka 13 imepita toka kifo chake kilichotokea Octoba 14, 1999.

Ikiwa Kanisa Katoliki lipo kwenye Mchakato wa kumtangaza Mwl. Julius Nyerere kuwa Mwenye kheri, Leo tumeona tuwakumbushe tukio hili la kihistoria lililofanyika katika viwanja vya jangwani Octoba 1990 baada ya Papa John Paul II kufanya Ziara Nchini Tanzania.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0QUyl3T3kGcCWc1zrZwG810N2Rq7gej_zgp8_yjouywpToXhFAXwtieerHh8jbRRjOBbItuo8cnjbYze9LBQdsQmXoc2GaKB5ixU6zvd9d6nyH_gg9qCURJiGn05G0o4eGvYUAoHEIaE/s1600/p2.jpg
Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere akipokea Sakramenti ya Meza ya Bwana toka kwa Papa John Paul II katika Viwanja vya Jangwani Octoba 1990, Papa huyo alipofanya ziara Nchini Tanzania. (Picha; Maktaba Yetu)