Advertise Here

Thursday, October 24, 2013

Askofu mbadhirifu afukuzwa Kanisani Ujerumani.

Askofu mbadhirifu afukuzwa kanisani Ujerumani
Vatican imemfuta kazi Askofu mmoja mbadhirifu wa Ujerumani. Makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani yamesema kuwa Vatican imechukua hatua hiyo kutokana na kiongozi huyo wa kanisa kufanya ubadhirifu.

Askofu Franz-Peter Tebartz-van Elst amefutwa kazi kwa kufanya ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za Kanisa. Kabla ya hapo, askofu huyo alikuwa analalamikiwa sana kwa kufanya ubadhirifu na watu walikuwa wanataka afukuzwe kwenye Kanisa Katoliki.

Katika taarifa yake, Vatican imesema kuwa, Kanisa Katoliki limemfukuza kwa muda Askofu Franz-Peter Tebartz-van Elst wa Limburg, Ujerumani. Taarifa zinasema kuwa, askofu huyo ametumia karibu Euro Milioni mbili na laki tisa kwa ajili ya kujenga makazi yake, fedha ambazo zilitoka kwenye mfuko wa kodi za masuala ya kidini wa Ujerumani.

Askofu huyo mwenye umri wa miaka 53 analaumiwa pia kwa kutumia Euro Milioni 31 kujengea eneo la Kanisa katika mji wa kale wa Limburg wakati gharama ya ujenzi wa eneo hilo ulikuwa ni Euro Milioni 5.5.

 - Iran Swahili Radio -