Advertise Here

Sunday, October 13, 2013

Mchungaji Joan Wairimu wa Kenya adai Talaka Mahakamani.

Mchungaji Joan Wairimu
Mwimbaji wa Nyimbo za injili toka nairobi kenya alitamba zaidi na wimbo wake wa Pambazuka na Yesu Mchungaji Joan Wairimu Githuku anataka kumtaliki mumewe Askofu William Musyoki Mwangangi huku kesi zao mbili zikiwa katika mahakama kila mmoja akimshutumu mwenzake kuwa ni Mzinzi.

Mchungaji Wairimu imeanzisha kesi hiyo katika mahakama ya Nairobi ambapo yeye anatafuta amri ya kujitenga na ndoa hiyo.

Nae mumewe Askofu William Musyoki Mwangangi akiomba mahakama kuvunja ndoa hiyo. Wanandoa hao walifunga ndoa Mwaka 1996.

Kesi yao hiyo imekuwa na shutuma mbalimbali kutoka ukatili, uzinzi, kuangalia sinema ya ngono, kunyimwa haki ya ndoa na utoaji wa vitisho vya kuuawa.

Mchungaji Wairimu ni mwanamuziki wa Nyimbo za injili anayevuma zaidi kwa wimbo wake wa Pambazuka na Yesu, wimbo ambao ni maarufu kwenye YouTube na uliopakuliwa(Download) Mara nyingi kama ringtone na Wakenya wengi. Pia anamiliki Pambazuka Production na Queens Ministry.

Askofu Mwangangi, ambaye ni Mkuu wa Kanisa la Jesus Manifestation Church la Githurai  amedai mke wake amemnyima haki yake ya unyumba tangu 2009.

Lakini Mchungaji Wairimu amekuwa akimshutumu Mumewe kujihushisha na Maswala ya uzinzi na wanawake tofauti tofauti akiwemo mfanyakazi wao wa ndani jambo linalomtesa kwa kuona Aibu.

Anadai kuwa Askofu ana mtoto wa nje ya ndoa pia kama matokeo ya vitendo vyake viovu, huku askofu akikana Madai hayo.


Hii ni video ya wimbo wa "Pambazuka na Yesu" wa Mchungaji Joan Wairimu

- Standard Media (Kenya) -