Advertise Here

Thursday, October 3, 2013

Happy Mkamwa ‘Nyatawe’ alilia Mtoto, Aamua Kuokoka.

MSANII wa maigizo kutoka Kundi la Msanii Afrika, Happy Mkamwa ‘Nyatawe’ ameamua kuokoka baada ya kuhangaika kwa muda mrefu akitafuta mtoto bila ya mafanikio.

Akizungumza kwa huzuni na paparazi wetu, Nyatawe ambaye anasali kwa Mchungaji Antony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ alisema kuwa yuko ndani ya ndoa kwa miaka mitatu lakini hajabahatika kupata mtoto na ameshahangaika katika hospitali mbalimbali.

“Kila tukichukuliwa vipimo na mume wangu, wote tunaonekana hatuna matatizo, pia nimetumia madawa ya kienyeji lakini hakuna mafanikio yoyote.

Kutokana na hilo msanii huyo ameona ni heri aokoke na kuwaomba wasanii wenzake wamuombee kwa sababu anatamani sana kuitwa mama.

“Nilishawahi kushika ujauzito lakini ukatoka na mpaka leo sijashika tena, mume wangu amekuwa akinifariji na kunipa moyo kwamba siku moja tutapata mtoto lakini nimekata tamaa,” alisema Nyatawe.

- Global Publishers -