Advertise Here

Sunday, October 13, 2013

Rais Mstaafu wa Kenya atoa Wito kwa Vijana kuishi Maisha Matakatifu.

Rais Mstaafu Daniel arap Moi
Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Moi
Rais mstaafu wa Kenya Daniel Moi ametoa wito kwa vijana kuishi maisha matakatifu ili waweze kuwa kwenye mstari wa mbele katika kuwasadia wengine kumjua Kristo. Moi ameyasema hayo mapema hii leo katika sherehe ya kuwabatiza wanafunzi wa shule mbali mbali za Msingi, Upili, na Vyuo vikuu katika kanisa la AIC Kabarak Community Chapel.

Aidha Moi amewataka vijana kuwa viongozi wema wa dini bila kuzingatia tofauti za madhehebu. Sherehe hii ya ubatizo ni ya ishirini na tano na hufanywa kila mwaka kwa watahiniwa ambao hupewa Biblia inayonuiwa kuwa mwongozo pindi wanapomaliza mitihani yao mwisho wa mwaka.