Advertise Here

Tuesday, October 22, 2013

Askofu: Waliofungwa China walijitakia Kifo.

Askofu Mkuu Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi mkoani Kilimanjaro, Isack Amani
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi Mkoani Kilimanjaro Isack Amani
ASKOFU Mkuu Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi mkoani Kilimanjaro, Isack Amani amesema watanzania 175 wanaoshikiliwa nchini China, kwa tuhuma za kufanya biashara ya dawa za kulevya, serikali haiwezi kuwaombea msamaha, kutokana na kutokuwa na mamlaka na serikali ya China.

Alisema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya shule ya Sekondari St. Amedeus, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Moshi, pamoja na kuzindua jengo la maabara ya sayansi.

Alisema serikali hawezi kuwaombea msamaha wa kutonyongwa watanzania wanaoshikiliwa kwenye magereza ya nchini China, kwani hawezi kuingilia sheria za nchi nyingine.

Alisema hakuna wa kulaumiwa, endapo watanzania hao watanyongwa, kwani wao ndio waliojitakia. Alieleza kuwa watuhumiwa hao wanatambua sheria za nchi hiyo vizuri, kwamba endapo mtu akikamatwa na dawa za kulevya, lazima anyongwe.

“Serikali haiwezi kuwaombea msamaha watanzania 175 wanaoshikiliwa nchini China kwa dawa za kulevya, sheria za nchi hiyo walizijua hivyo walijitakia wenyewe, pia serikali yetu haina mamlaka kwenye sheria za China,” alisema Askofu Amani.

“Hakuna umuhimu wa serikali kuwaombea wasinyongwe, wamejitakia wenyewe kifo kwani wanajua vyema kule kuna sheria kali, na sisi hatuna mamlaka na huko hivyo serikali yetu haina cha kufanya,”alisema.

Alisema serikali wakati ikishererekea miaka 50 ya uhuru inapaswa kutatua tatizo la ajira kwa kuweka mazingira mazuri kwa vijana ili wasiweze kujiingiza kwenye matukio ambayo yanawagharimu uhai wao.

Akofu Amani alifafanua kwamba wakati serikali ikipigana na adui maradhi, ujinga na umaskini, pia itambua upougonjwa wa dunia wa uaminifu na kutojali amri za Mungu, maadili katika jamii, hali inayosababisha taifa kuyumba kutokana na kukosekana kwa haki.

- Habari Leo -